Toleo hili jipya limejaa maboresho ya udhabiti na utendajikazi, na tumeanzisha vipengee vipya ili kufanya kuvinjari kwako bora zaidi na rahisi zaidi.
Hifadhi kurasa zako unazozipenda kwa kubofya. Sasa unaweza kuongeza kurasa kwa Vialamisho au Upigaji Haraka papo hapo, kwa kuteua nyota katika uga wa anwani.
Uga wa anwani ya Opera pia umeboreshwa na mapendekezo mapya ya utafutaji, kwa hivyo kuifanya rahisi kuona tovuti zako uzipendazo kwenye orodha.
Pamoja na kiasi cha maboresho kwenye mtambo wa kivinjari, Opera 11.60 hujumuisha programu mpya inayotangamana na HTML5. Hii huwapa watengenezaji wavuti utendajikazi tondoti na utangamanifu ulioboreshwa na vivinjari vingine.
Kwa kuongezea, huduma yetu ya barua iliyojengewa ndani imeboreshwa na muundo mpya na urambazaji wenye kuhisi zaidi.
Tafadhali tembelea Ni nini kipya ikiwa unataka maelezo zaidi juu ya kisasisho hiki.